Newala FM

MWENGE WA UHURU WAWASILI WILAYANI LUDEWA

MWENGE WA UHURU WAWASILI WILAYANI LUDEWA

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa- Victoria Mwanziva na uongozi mzima wa Ludewa upande wa Chama na Serikali- sambamba na Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga, wameungana na wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wakiongozwa na Comrade Godfrey Mnzava kuukimbiza Mwenge wa Uhuru Wilayani Ludewa.

 

Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa umbali wa Kilometa 93 Wilayani Ludewa; ukipitia Miradi 7 yenye thamani ya Jumla ya Tsh 8,721,001,010.35
Miradi hii ya Maendeleo ni miradi ya Sekta za Afya, Maji, Elimu, Miundombinu- Mazingira.

 

Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024:
“Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”