MTWARA.
Wazazi na walezi wamehimizwa kuwapeleka watoto shuleni
Kupata Elimu kwani serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na raisi dkt.Samia Suluhu Hassan KWENDA imepunguza gharama kubwa Kwa mzazi.
Hayo Yamezungumzwa Tarehe 14/9/2024 na Mgeni Rasmi Mwl.Diana Sonno Ambae pia ni mkuu wa idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya mji Newala kwenye Tamasha la kupinga Ukatili wa jinsia
Lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la SPORT DEVELOPMENT AIDS (SDA) na kufanyika kwenye Kijiji Cha Mahumbika kilichopo Halmashauri ya mji Newala mkoani Mtwara
Aidha Afisa mwezeshaji kutoka shirika la spots development aids (SDA) wilaya ya Newala ndg.Denis Fikili kwa niaba ya shirika ametoa shuklani kwa wadau wote wa elimu na michezo kwa ushirikiano kwani wanaendelea kupiga hatua kuhakikishan watoto wanatimiza ndoto zao
Kwa upande wa mkaguzi msaidizi wa polisi lakini pia ni mkuu dawati la jinsia na watoto wilaya ya Newala Afande Tumaini Ngwanda
Amewataka wazazi kuendelea kuwa walinzi Kwa Watoto wao.
Kulingana na Elimu zilizotolewa kwenye Tamasha Hilo Baadhi ya wanafunzi na wazazi wameelewa namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili .