Wakulima wa chama kikuu Cha ushirika Tandahimba na Newala (Tanecu Ltd) wamekubali kuuza zao La Ufuta Kwa bei ya juu 3,203 na bei ya chini 3,203.
Hayo yamejiri June /21/2024, katika mnada wa 02 uliofanyika katika kijiji cha Chitandi (SHIMO LA MUNGU AMCOS) Halmashauri ya Mji Newala ambapo, jumla ya Tani 330 na kilo 483 zimeuzwa huku kampuni 01 pekee ndiyo iliyojitokeza kununua ufuta huo.